Suge Knight akimbizwa hospitali

0
660

Suge KnightLOS ANGELES, MAREKANI
KIONGOZI wa kundi la Death Row Records, Marion Hugh ‘Suge Knight’, amekimbizwa hospitali mara baada ya kuzidiwa na tumbo akiwa jela.
Msanii huyo kwa sasa anatumikia kifungo kwa kumgonga mtu na gari na kusababisha kifo chake.
Mara kwa mara msanii huyo amekuwa akipata ugonjwa anapofikishwa tu mahakamani ama siku za karibu za kwenda mahakamani zinapokaribia.
Mtandao wa TMZ umeeleza kwamba msanii huyo amekuwa akipata matatizo ya afya kwa kuogopa miaka ya kifungo chake, hadi sasa hajui kifungo chake kitakwisha lini, hivyo anapata presha siku anapofikishwa mahakamani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here