27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

50 Cent auza nyumba ya vyumba 52

50 CentNEW YORK, MAREKANI
RAPA 50 Cent ameshangaza watu kwa kuamua kuuza nyumba yake yenye vyumba 52 kwa thamani ya dola milioni 8.
Msanii huyo wa wimbo wa ‘Candy Shop’, mwaka 2007 alitangaza kuiuza nyumba hiyo kwa kitita cha dola milioni 18.5, lakini sasa ameiuza kwa dola milioni 8, pungufu kwa dola milioni 10.5.
Hata hivyo, thamani ya nyumba hiyo ilionekana kushuka kila mwaka tangu alipotangaza kuiuza mwaka 2007.
Nyumba hiyo mbali ya kuwa na vyumba 52, kuna sehemu ya kiwanja cha mpira wa kikapu, ukumbi wa muziki, Casino na sehemu ya kupaki helikopta.
Msanii huyo kwa sasa amekuwa na wakati mgumu tangu kuuzwa kwa nyumba hiyo kutokana na kupokea lawama za mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles