26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Stars yaichapa Madagascar, yakaa kileleni

Na Mohammed Ulongo, Mtanzania Digital

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeichapa Madagascar mabao 3-2 na kukaa kileleni mwa Kundi J katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar.

Katika mchezo huo uliochezwa leo Septemba 7 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, mabao ya Taifa Stars yamefungwa na Erasto Nyoni (dk. 2) kwa mkwaju wa penalti, Novatus Dismas (dk. 26) na Feisal Salum ‘Fei Toto’ (dk. 76), huku yale ya Madagascar yakifungwa na  Njiva Rakotomarimalala (dk. 36) na Thomas Fontaine (dk. 45).

Novatus Dismas na Saimon Msuva wakishangilia bao alilofunga

Matokeo hayo yanaifanya Stars kuonga kundi  J, baada ya kufikisha pointi nne sawa na Bennin iliyo nafasi ya pili zikitofauti idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, wakati nafasi ya tatu ni DR Congo yenye alama mbili, huku Madagascar ikiwa haina pointi yoyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles