Mohamed Kassara – Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije, ameita kikosi cha wachezaji 35, kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika (Afcon) dhidi ya Tunisia na fainali ya Mataifa Afrika kwa Wachezaji Wanaocheza Ligi za Ndani (Chan).
Kikosi hicho kinatarajia kuingia kambini kesho na kuanza kujifua kwa ajili ya kuumana na Tunisia na baadaye kutimkia Cameroon kushiriki Chan, ambayo inatarajia kuanza Aprili 4 hadi 25.
Stars ilikata tiketi ya kushiriki Chan, baada ya kuitoa Sudan kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-2, ikianza kufungwa bao 1-0 nyumbani, kabla ya kushinda mabao 2-1ugenini.
Ndayiragije anakuwa kocha wa pili kuipeleka Stars katika michuano hiyo, baada ya Mbrazil, Marcio Maximo aliyeifikisha katika fainali za mwaka 2009 zilizofanyika nchini Ivory Coast.
Kikosi hicho kiundwa na walinda mlango, Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Yanga), David Kisu (Gor Mahia, Kenya) na Salum Salula (Malindi, Zanzibar).
Mabeki ni Somari Kapombe na Mohammed Hussein (Simba), Juma Abdul (Yanga),Kelvin Kijiri (KMC),Nickson Kibabage ( Diffa El Jadid ,Morocco), David Bryson (Gwambina, Abdi Banda ( Highlandspark, Afrika Kusini), Bakari Nondo (Coastal Union), Agrey Moris (Azam), Dikson Job(Mtibwa Sugar), Kelvin Yondan na Said Makapu (Yanga), na Erasto Nyoni (Simba).
Viungo, Jonas Mkude (Simba, Feisal Salum (Yanga),Himid Mao (ENNPI, Misri), Brayson Raphael na Abubakari Salum (Azam), Hassan Dilunga (Simba), Reliants Lusajo (Namungo),Ayub Lyanga (Coastal Union), Sixtus Sabilo (Polisi Tanzania), Balama Mapinduzi (Yanga).
Washambuliaji, John Bocco (Simba), Ditram Nchimbi (Yanga), Mbwana Samatta (Aston Villa, England), Lucas Kikoti (Namungo), Shaban Chilunda (Azam), Farid Mussa (FC Tenerrif, Hispania), Simon Msuva(Diffa El Jadida, Morocco) na Iddi Seleman, Azam.