Na Grace Shitundu-DAR ES SALAAM
STAILI ya Rais Dk. John Magufuli kuteua, kupanga, kupangua na kutumbua mara kwa mara watendaji wake, imeelezwa na wasomi kuwa ni ya kipekee na ambayo haijawahi kutekelezwa na yeyote nchini.
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake, tayari Rais Magufuli amewaondoa mawaziri 15 katika safu yake, huku Mamlaka ya Mapato (TRA) ikiongozwa na makamishna watano hadi sasa.
Pia katika kipindi hicho amebadilisha mara kadhaa safu ya watendaji wake katika ngazi mbalimbali kwa kuwateua wengine wapya, kuwahamisha na kuwaondoa baadhi.
Staili hiyo imeonekana kuzua mjadala baada ya juzi Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Steven Kebwe na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loata Sanare, sambamba na kujaza nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi.
Sanare anachukua nafasi ya Dk. Kebwe, ambaye hivi karibuni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimnyooshea kidole kwa kushindwa kuwasimamia watendaji walio chini yake baada ya kuwepo upotevu wa fedha.
Mbali na Majaliwa, Rais Magufuli yeye mwenyewe na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally kwa nyakati tofauti nao walipata kumwonya Dk. Kebwe kwa kushindwa …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.