32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

SOMALIA WACHAGUA RAIS KATIKATI YA MILIO YA RISASI

MOGADISHU, SOMALIA

MILIPUKO imesikika katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu usiku wa kuamkia jana, wakati wabunge wakijiandaa kumchagua rais mpya.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya kuahirishwa mara kadhaa tangu Agosti mwaka jana kutokana na vitisho vya mashambulizi kutoka wanamgambo wa Al-Shabaab

Sauti za mizinga zilisikika karibu na na Uwanja wa Ndege wa Mogadishu, ambako uchaguzi huo ulifanyika, huku wakazi wa eneo la Waberi lililoko Kusini Magharibi mwa Mogadishu wakithibitisha kusikia milipuko hiyo.

Kufikia sasa hakuna vifo au majeruhi walioripotiwa ingawa hali ya wasiwasi imetanda mjini hapa, ambako bababara zote muhimu zimefungwa huku kukiwa na marufuku ya ndege kuruka.

Awali uchaguzi ulikuwa ufanyike katika Chuo cha Polisi kabla ya kuhamishwa katika uwanja huo wenye ulinzi mkali kutokana na kile kilichoelezwa tishio la usalama na kukithiri kwa rushwa katika chuo hicho.

Wabunge na maseneta walishuhudiwa wakikusanyika nyuma ya majengo ya uwanja wa ndege, ambao unalindwa vikali na majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika (AMISOM).

Eneo hilo ndiko yaliko pia mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na balozi za kigeni.

Awali uchaguzi huo ulianza kwa kuwachagua wazee na watu maarufu wa kikanda 14,000, wabunge 275 na maseneta 54, ambao ndio waliotarajia kuamua kumuunga mkono Rais Sheikh Mohamud au wamchague mmoja kati ya wapinzani wake 21.

Mwangalizi wa uchaguzi huo na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Mohamed Shire, alisema ni jambo jema uchaguzi huo unafanyika na hiyo ni hatua kubwa kwa wananchi wa Somalia ukizingatia pia jumuiya ya kimataifa inaunga mkono.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles