19.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

Simbachawene aonya mabasi 16 yanayovunja sheria

Na Mwandishi Wetu-MoHA, Dodoma

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameyaonya  mabasi 16 ya abiria yanayofanya safari zake katika mikoa mbalimbali nchini kuacha mara moja tabia ya kuvunja Sheria za Usalama Barabarani zinazohatarisha maisha ya Watanzania wanaotumia huduma hizo za usafiri.

Simbachawene, ametoa onyo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kuhusu hali ya usalama na matukio ya ajali za barabarani hapa nchini hususan katika kipindi hiki tunapoelekea Sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.

Mabasi yaliyoonywa ni pamoja na T367 ARH-Asante Rabbi yanayofanya safari zake za Arusha kuelekea Mwanza, T498 BYZ-Kidia One linalotoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam, T395 BAP-Asante Rabbi linalotoka Arusha kuelekea Mwanza, T718 DPK-Maning Nice linalotoka Morogoro kuelekea Masasi, T695 DMJ-Ally’s Star linalotoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza, T424 AWB-Mgamba linalotoka Mwanza kuelekea Arusha, T253 DHM-Capricon linalotoka Arusha kuelekea Mbeya, T400 AKM-Yellow line linalotoka Singida kuelekea Mbeya.

Simbachawene ameyataja mabasi mengine kuwa ni, T756 DNT-Ally’s Star linalotoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam, T260 DUC-Frester linalotoka Dar es salaam kuelekea Mwanza, T221 DKB-Saratoga linalotoka Dar es Salaam kuelekea Kigoma, T988 AHB-Capricon, T450 AWJ-Frester, T774 DRL-BM linalotoka Arusha kuelekea Dar es Salaam, T768 DRL-BM linalotoka Arusha kuelekea Dar es Salaam, T775 DRL-BM linalotoka Arusha kuelekea Dar es Salaam.

Simbachawene, amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mabasi yote yanayokiuka Sheria za Usalama Barabarani;

“Nimesema nitachukua hatua kali za kisheria  kwa ajili ya mabasi yote  niliyoyataja na yote yatakayobainika kuvunja Sheria zote za Usalama Barabarani, na hili nalisema kwa uwazi kabisa madereva acheni kuhatarisha maisha ya Watanzania” alisema Simbachawene.

Simbachawene amesema takwimu  zinaonyesha kuwa chanzo kikubwa cha ajali za barabarani ni pamoja na makosa ya kibinadamu, ubovu wa vyombo, mwendokasi yaani madereva kuendesha magari au vyombo vya moto kwa mwendo kasi kinyume cha sheria.

Aidha, Simbachawene ameeleza hali ya Usalama kwa kipindi cha Januari hadi Novemba, 2020 ni nzuri ambapo uhalifu umedhibitiwa kwa kiwango kikubwa, “Pamoja na kuwepo kwa uhalifu wa makosa madogo madogo yanayoendelea kujitokeza, Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuyapunguza makosa hayo” alisema Simbachawene.

“Kwa upande wa Usalama Barabarani, takwimu za ajali  barabarani kuanzia Januari, 2019 hadi Novemba, 2021 zinaonyesha idadi ya ajali, vifo na majeruhi zinaendelea kupungua” alisema Simbachawene

Vilevile, Simbachawene ameeleza takwimu za mwaka 2020 zinaonyesha kuwa kuna upungufu wa ajali 921 ambayo ni asilimia 37, vifo 194 sawa na asilimia 14 na majeruhi 636 ambayo ni sawa na asilimia 24 kulinganisha na Mwaka 2019.   

Simbachawene ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia na kupambana na uhalifu na kuzuia ajali za barabarani kwa kutii sheria bila shuruti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,459FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles