26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yazipiga jeki shule za sekondari Kasulu

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Benki ya NMB imekabidhi mabati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 11.2 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa kwenye shule za sekondari mbili wilayani Kasulu.

Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi  – Sospeter Magesse (wa pili kushoto) akikabidhi sehemu ya mabati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Waziri wa elimu elimu, sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (katikati) kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madara ya shule ya sekondari Ruhita na Kidiama wilayani Kasulu mkoani mkoani kigoma. Mabati hayo yalikabidhiwa kwenye hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari Ruhita.

Mabati hayo yalikabidhiwa kwa Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako kwa niaba ya shule za sekondari Ruhita na Kidiama kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo.

Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika juzi katika shule ya sekondari Ruhita.

Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magesse alisema kuwa wamekabidhi mabati hiyo ikiwa ni kuunga mkono mkakati wa serikali kuhakikisha wanafunzi wote waliomaliza darasa la Saba na kufaulu wanajiunga na sekondari mwezi Januari mwakani.

Magesse alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa kutoa misaada kwenye shughuli mbalimbali ya kijamii ikiwa ni kurudisha shukrani kwa jamii kutokana na michango mkubwa ulioifanya benki hiyo kupata mafanikio.

Akizungumza katika Mkutano huo, Waziri wa elimu, sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameshukuru benki ya NMB kwa msaada huo ambapo ametoa agizo kwa maafisa elimu nchini kote kusimamia ujenzi wa madarasa hayo na kuhakikisha madarasa yanamalizika na wanafunzi wanapata nafasi.

Pamoja na hilo, Waziri Ndalichako amewaonya wakuu wa mikoa kutojiingiza kwenye mtego wa kupika taarifa kuhusu upungufu na ukamilishaji wa madarasa na wale watakaobainika kutoa taarifa za uongo hatua za kinidhamu zitachukuliwa.

Awali, Mkuu wa wilaya Kasulu, Simon Hanange alisema kuwa jumla ya wanafunzi 3500 wamefaulu darasa la saba mwaka huu na Mipango iliyopo ni kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanajiunga na sekondari Januari mwakani.

Hanange alisema kuwa hadi sasa vyumba vya madarasa 75 vipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji na kwamba kufikia Februari mwakani vyumba vyote vitakuwa vimekamilika na kutumikia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles