33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mifuko ya Hifadhi za Jamii yatakiwa kupunguza matumizi

Na Sheila Katikula, Mwanza

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amezitaka bodi kusimamia matumizi ya yasiwe makubwa kwenye mifuko ya sekta ya shirikisho la mashirika ya hifadhi ya Jamii nchini ili yasizidi matumizi  na kupelekea kushindwa kufikia malengo ya kutoa mafao kwa wanachama.

Waziri huyo, ametoa wito huo leo Desemba 22, jijini Mwanza wakati wa kufunga mkutano wa jumbe wa shirikisho la mashirika ya hifadhi ya Jamiii nchi (TSSA) amesema bodi inajukumu la kushauri na kusimamia uwekezaji unaofanywa na  mifuko ya hiyo  kwa lengo la kulinda fedha za wanachama.

Amesema mifuko ya hifadhi ya jamii inajukumu la kushauri  na kuona  kwenye viwanda vinyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi hapa nchi na siyo kuagiza nche ya nchi  kwani ni vema  kuanzisha vya hapa nchini amvavyo vitakavyotoa ajira na kuongeza idadi ya wanachama vitakavyosaidia kupanua wigo wa sekta hiyo.

“Inasikitisha kuona hata dripu la maji ya kumwekea mgonjwa  tunashindwa kuzalisha tunaagiza kutoka nje wakati uwezo wa kuanzisha viwanda tunao nitafarijika zaidi nitakapo sikia  kuwa malengo haya  yametimizwa na viwanda hivyo vinatoa ajira kwa vijan,” amesema Mhagama.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto,  Prof. Mabula Mchembe ameishukuru TSSA kwa kutoa mafunzo  hayo ya siku tatu yenye lengo la kutambua jinsi ya uendeshaji  wa mfuko ya hifadhi ya jamii katika uwekezaji wa viwanda.

Aidha, Mwenyekiti wa TSSA, William Erio  amesema watafanya mpango wa kufufua kiwanda cha nyama cha Busisi  ili kiweze kufanya kazi na vijana  waweze kupata ajira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles