EU waidhinisha mauzo ya chanjo BioNTech-Pfizer

0
772

Brussels, Ubelgiji

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imeidhinisha kwa masharti mauzo ya chanjo iliyotengenezwa na kampuni ya Pfizer ya Marekani kwa ushirikiano na kampuni ya Ujerumani, BioNTech. Rais wa Halmashauri hiyo, Ursula von der Leyen, amesema akiwa mjini Brussels kwamba hii ni hatua muhimu katika juhudi za kuutafutia dawa ugonjwa wa COVID-19.

Hiyo ni chanjo ya kwanza dhidi ya virusi vya corona kuidhinishwa na Umoja wa Ulaya. Itaanza kutolewa katika mataifa tofauti ya Ulaya mwezi huu. Nchini Ujerumani, wananchi wataanza kudungwa chanjo hiyo mnamo Decemba 27.

Wafanyakazi wa huduma za afya na watu wengine walio katika hatari kubwa, tayari walianza kupewa chanjo hiyo ya BioNTech-Pfizer nchini Uingereza na Marekani, jambo ambalo limezishinikiza serikali za mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya kuchukua hatua za haraka zaidi kuliko walivyopanga hapo awali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here