21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Simba kumlipa Kwizera

PIERRE KWIZERANA SAADA SALIM, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa klabu ya Simba umeamua kumlipa aliyekuwa mchezaji wake, Pierre Kwizera, Sh 8,880,000 (sawa na Dola 4800 za Marekani) kati ya Sh 17,760,000 inazodaiwa.
Kwizera alisajiliwa na Rayon Sport ya Rwanda baada ya Simba kuvunja mkataba wake huku nafasi yake ikichukuliwa na Mganda, Simon Sserunkuma.
Kiungo huyo ameliambia MTANZANIA kuwa amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope na tayari amelipwa nusu ya fedha ambazo alikuwa akidai na baadaye atamaliziwa.
Alisema baada ya kuwapigia simu mara kadhaa viongozi wa klabu hiyo bila mafanikio, alitishia kwenda Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuishtaki klabu hiyo.
“Sikukata tamaa juu ya kufanya mawasiliano na viongozi kwani awali nilipewa namba ya Kassim Dewji na baadaye Hanspoppe ambapo amenipa maelekezo ya kwenda kuchukua fedha hizo Burundi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles