MKURUGENZI wa Tamasha la Ziff, Profesa Martin Mhando, amesema kwamba baadhi ya filamu katika tamasha la mwaka huu zitatumika kwa ajili ya kufundishia.
“Tumeanza kujihusisha na filamu za kuonyesha vijijini na kufundishia shuleni ambapo shule zaidi ya 25 zitanufaika kwa elimu hiyo itakayokuwa ikitolewa kila wiki.”
Alisema wameona kuna umuhimu mkubwa kutumia filamu kufundishia ili kuongeza mwamko wa wanafunzi na wakazi wengi wa vijijini kuzifahamu filamu na kuelewa kwa haraka.
“Filamu hizi baada ya kuzitazama, kuna wataalamu wanakaa na wana kijiji na wanafunzi wanajadili namna walivyoelewa na watakavyowaelekeza mambo mbalimbali kwa kuwa filamu zenyewe ni za mafunzo maalumu,” alieleza.