29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mbio za ngalawa zapata washindi

Mshindi wa kwanza wa mbio za  Ngalawa.
Mshindi wa kwanza wa mbio za Ngalawa.

NA FESTO POLEA,

WASHINDI watatu wamepatikana katika mbio za ngalawa zilizofanyika visiwani Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa Tamasha la ZIFF.

Mbio hizo zilijumuisha ngalawa 12 lakini tatu ndizo zilizofanikiwa kuwahi kurudi lilipoanzia shindano kwa haraka kuliko nyingine huku ngalawa mbili zikifungana nafasi ya tatu.

Washindi hao na ngalawa zao kwenye mabano ni iliyoshika nafasi ya kwanza iliyokuwa chini ya nahodha, Haji Hassan Kondo, (Kindumbwendumbwe), aliyeshika nafasi ya pili, iliongozwa na nahodha, Mhidin Sadi (Kesho tena) na walioshika nafasi ya tatu ni washindi wawili ikiwemo iliyoongozwa na nahodha, Abrahaman Omary (Dragon) na iliyoongozwa na Suluhu Hassan (Ipo Vipi).

Mratibu wa Tamasha hilo, Sabrina Othuman, alisema mashindano hayo bado yamekosa udhamini wa kuwezeshwa kufanyika maeneo mengine ya pwani kama walivyojaribu kufanya kwa mwaka uliopita.

“Ni mashindano mazuri lakini tunakosa wadhamini kwa kuwa lengo letu ni kufanya maeneo mengi ya pwani ili tupate washiriki wengi kutoka mikoa mbalimbali, siku ya tamasha tunawashindanisha na kupata washindi watatu kama tulivyopata leo,” alisema Sabrina.

Naye Waziri wa Afya Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo, aliwataka washindi hao kuongeza juhudi za uendeshaji wa ngalawa hizo na fedha walizopata katika kukuza uchumi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles