Jeremia Ernest
Shirikisho la korosho Afrika (ACA), linategemea kukutana na wadau mbalimbali kwenye Mkutano wa 13 wa korosho mwanzoni mwa mwezi novemba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wahabari mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Dk. Steven Ngairo, amesema Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es salaam.
“Lengo la kukutana na wadau katika Mkutano huo ni kuendeleza ushirikiano na Kushawishi mabadiliko katika soko,” amesema Dk. Ngairo
Amesema kuwa mwaka huu wana lengo la kuchambua mabadiliko ya sasa ya soko, mwitikio wa serikali na watendaji wa mnyororo wa thamani na kuchanganua wajibu wa wadau wote wa umma na binafsi katika kushughulikia masuala yanayojitokeza .
Pia ametoa wito kwa wadau wote kuunga mkono mkutano huo kwa washiriki na kujadili mustakabali wa tasnia ya Korosho bara la Afrika kwa ujumla.