24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Shirikisho la korosho Afrika kukutana na wadau Novemba

Jeremia Ernest

Shirikisho la korosho Afrika (ACA), linategemea kukutana na wadau mbalimbali kwenye Mkutano wa 13 wa korosho mwanzoni mwa mwezi novemba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wahabari  mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Dk. Steven Ngairo, amesema Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es salaam.

“Lengo la kukutana na wadau katika Mkutano huo ni kuendeleza ushirikiano na Kushawishi mabadiliko katika soko,” amesema Dk. Ngairo

Amesema kuwa mwaka huu wana lengo la kuchambua mabadiliko ya sasa ya soko, mwitikio wa serikali na watendaji wa mnyororo wa thamani na kuchanganua wajibu wa wadau wote wa umma na binafsi katika kushughulikia masuala yanayojitokeza .

Pia ametoa wito kwa wadau wote kuunga mkono mkutano huo kwa washiriki na kujadili mustakabali wa tasnia ya Korosho bara la Afrika kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles