22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawatoa hofu wakulima ununuzi wa pamba

ALLAN VICENT, TABORA

Serikali imewahakikishia wakulima wa zao la pamba nchini kuwa pamba yao yote iliyovunwa msimu huu itauzwa bila kizuizi chochote na kwamba wanunuzi wako tayari.

Hayo yamebainishwa leo jumanne Julai 16, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Mwabakima kata ya Mbutu wilayani Igunga Mkoani Tabora.

Amesema amekutana na wanunuzi wa zao hilo hapa nchini na wamekubaliana pamba yote iliyorundikana katika maghala ya vyama vya msingi vya wakulima (AMCOS) inunuliwe.

Amesema serikali imesikia kilio cha wakulima wa pamba ndio maana imeagiza Gavana wa Benki Kuu kutoa kibali kwa mabenki makubwanchini kukopesha wanunuzi ili pamba yote inunuliwe kwa fedha taslimu na sio mkopo.

Aidha Majaliwa ameeleza bayana kuwa serikali haiwezi kuendelea kuwagawia wakulima hao pembejeo za bure hivyo amewataka kutumia vizuri fedha wanazolipwa ikiwemo kujiwekea akiba kwa ajili ya kununulia pembejeo kwa msimu ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles