Remtullah awashukuru wadau wa mtindo kwa kumpa ushirikiano

0
948

Jeremia Ernest

Mbunifu maarufu wa mavazi nchini, All Remtullah, amewashukuru wadau wa mitindo nchi kwa kumpa ushirikiano katika tasnia tangua ajitambulishe mwaka 2007, ambapo kwa mafanikio aliyoyapata ameamua kuandaa tamasha la kuonyesha mavazi ya kitenge litakalofanyika jumamosi Julai 20, katika uwanja wa Mnazi mmoja.

Remtullah amekua akivalisha watu mbalimbali mashuhuri wakiwemo wasanii, wanasiasa na kampuni kubwa hapa nchini.

Akizungumza na Bingwa amesema anawashukuru wadau pamoja na wanahabari kwa kuendelea kumuunga mkono katika kazi zake.

“Ni miaka 12 sasa tangu nimeanza kufanya kazi ya ubunifu nimepata mafanikio makubwa kwa kushikwa mkono na wanahabari pamoja na wadau wa mitindo” amesema Remtullah.

“Nimeamua kuandaa onyesho na litakua la kwanza hapa nchini kufanya, kukiwana na muitikio mzuri litakuwa ni endelevu,” Remtullah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here