Mwandishi Wetu, Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amepokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona na kuwataka wafanyabiashara wengine kuguswa na kuchangia ili kuhakikisha wanadhibiti maambukizi mkoani humo.
Shigela amesema hayo leo wakati akipokea msaada wa matanki matano yenye ujazo wa lita 500 kila moja kutoka kampuni ya vifaa vya ujenzi ya Hussein plastic Industry ya Jijini Tanga.
Amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo katika maeneo mengi mkoani humo.
“Licha ya kwamba bado kama mkoa hakuna mgonjwa hata mmoja lakini tumeona iko haja ya kuendelea kutii maagizo ya wataalamu wa afya juu ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo,” amesema Shigella.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Yusuf Tayabali amesema wameamua kutoa msaada huo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano ya ugonjwa huo.