31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SHEIN ATANGAZA NEEMA KWA WATUMISHI

MAULI MUYENJWA NA LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


 

dr. sheinZANZIBAR imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi   huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali za maendeleo na utoaji wa huduma bora za  jamii, imeelezwa.

Akihutubia kwenye maadhimisho hayo jana, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein alitangaza nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa umma ambako kima cha chini sasa kitakuwa Sh 300,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100.

Alisema  katika sherehe hizo zilizofanyika Uwanja wa Amani Mjini Unguja, Dk. Shein alisema kiasi hicho kimepanda kutoka kima cha chini cha Sh 150,000 kwa mwezi.

“Hivi karibuni mshahara mpya utaanza kulipwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 100.

“Sasa watumishi wa umma watapata fedha hizo zitakazowasaidia  kupata maendeleo yao na taifa kwa ujumla,” alisema Dk. Shein.

Dk.Shein alisisitiza msimamo wa Serikali wa kuendelea kubana matumizi kwa kudhibiti safari za nje, posho za vikao na semina kutokufanyika hotelini.

Rais huyo wa Zanzibar alimpongeza Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisema  ushirikiano wake   umeiwezesha Zanzibar kupata uhalali wa kutafuta na kuchimba   mafuta na gesi.

Kuhusu umuhimu wa Mapinduzi, alisema   siku hiyo ni muhimu katika historia ya Zanzibar kwa sababu  ndiyo  ambayo Wazanzibari walikuwa huru katika nchi yao na kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maaendeleo.
“Tukiwa tunasherehekea miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni vema tukajivunia maendeleo yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana.”alisema Dk. Shein.

Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu Mapinduzi  yatokee Januari 12 1961, Dk. Shein alisema   mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta za elimu kwa kuwa na ongezeko la shule kutoka 752 mwaka 2015 hadi kufikia 843 mwaka 2016.

Ongezeko hilo limeenda sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi   kutoka 384,000 hadi kufikia 424,000 mwaka 2016.

Alisema katika sekta ya afya yamekuwapo mafanikio ya kuongezeka vituo vya afya kwa asilimia 13.4.

Dk. Shein alisema  mwaka 2015 kulikuwa na vituo 134 vya sasa na sasa viko vituo 152.

Mafanikio mengine ni   upatikanaji wa ajira 2,658 zilizotokana na miradi mbalimbali iliyozinduliwa katika kipindi hiki cha maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi, kukua kwa sekta ya utalii kwa ongezeko la watalii kwa asilimia 13 huku ikichangia pato la taifa kwa asilimia 27.

Huduma za  jamii nazo zimeboreshwa huku upatikanaji wa maji safi na salama umeendelea kukua ambako miradi ya maji imekuwa ikitekelezwa kwa kasi ikiwamo kuchimba visima vipya tisa na kuvifanyia ukarabati vya zamani.

Naye  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd alisema   Mapinduzi hayo yamekuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuwa yamewaweka Wazanzibari kuwa huru katika kutekeleza shughuli zao.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles