25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA: CCM INA WEWESEKA

Na Mwandishi Wetu-KAHAMA


 

Edward LowassaWAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amesema kasi ya kuimarika kwa umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani nchini, kunaitia kiwewe CCM kiasi cha kuanzisha mbinu chafu za kisiasa.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Kahama katika Hoteli ya Gaprina ambapo alifikia kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Kagera katika ziara ya kuimarisha chama chake.

Alisema kuimarika kwa mshikamano huo chini ya mwavuli wa Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi  (Ukawa) ni hatua kubwa katika kuelekea kuing’oa CCM.

“Wameanza mbinu zao za kutaka kutuondoa katika umoja wetu, wameanza kuwalisha viongozi wetu maneno, mfano  gazeti (nalitaja jina) la leo (jana) wamenilisha maneno ya kwamba eti nimeitabiria CCM ushindi katika uchaguzi mdogo wa udiwani kule Arumeru.

“… mambo ya ajabu kabisa hili  gazeti linaishi kwa kodi zetu sisi wananchi leo linaamua kutumika kuvunja demokrasia inasikitisha sana.

“Wanaandika uongo mchana kweupe kuwa nilikuwa katika kampeni kwenye kitongoji Ematasia..mimi sikwenda huko..lakini mbinu zao hizi wananchi wameshazijua na hawako tayari kuona hamu yao ya kupata mabadiliko inapotea,” alisisitiza.

Wakati huo huo mamia ya wakaazi wa mji wa Kahama waliizingira Hoteli ya Gaprina alikofikia Lowassa, wakiwa na nia ya kutaka kumwona.

Akiwa njiani kuelekea Bukoba, Lowassa na msafara wake alipata nafasi ya kusalimiana na wananchi katika mnada wa Lusaunga wilayani Biharamlo, ambako wananchi hao walimwambia kuwa hali yao ya maisha ni ngumu pamoja na hali mbaya ya ukame inayowakabili.

Hata hivyo Lowassa hakutoa kauli yoyote kwao zaidi ya kusema kwa sasa mikutano ya hadhara imepigwa marufuku na asingependa kuvuja sheria kwa kile alichodai amri kandamizi.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles