23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yavunja mkataba na Mkandarasi mradi wa maji Same

Na Mwandishi Wetu,Mwanga

Serikali imevunja mkataba na Mkandarasi aliyekuwa akitekeleza mradi mkubwa wa maji wa Same, Mwanga na korogwe, kutokana na kushindwa kuukamilisha kwa wakati.

Mradi huo ambao umegharimu zaidi ya Sh bilioni 262, ulipaswa kukamilika Mwaka 2017 na kuhudumia jumla ya wananchi 438,000.

Waziri wa maji, Jumaa Aweso alisitisha mkataba huo na kampuni ya M.A Kharafani ya nchini Misri baada ya kutembelea na kukagua mradi huo, wilayami Mwanga, Mkoani Kilimanjaro.

Alisema serikali imefikia maamuzi ya kuvunja mkata huo na mkandarasi Kharafi kutokana na kushindwa kuukamilisha kwa miaka zaidi ya mitatu ambapo ulipaswa kukabidhiwa Julai, 2017.

“Wizara haina sababu ya kusuasua huku wananchi wakiendelea kukosa maji huku pesa zikiwepo…hivyo tumesitisha rasmi mkataba wa mkandarasi ambaye allikuwa katika eneo la chanzo,wizara inafanya utaratibu wa haraka wa kutafuta njia ya kufanya wananchi wapate maji,@ alisema Aweso.

Alisema wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani pamoja na mamlaka nyingine ikiwemo shirika la umeme nchini TANESCO watahakikisha wanakamilisha mradi huo.

Katika hatua nyingine, Aweso amemtaka Mkandarasi Badr East Africa Enterprises LTD kuongeza kasi ya utekelezaji katika mkataba wake na kwamba ifikapo Machi, 2021 akabidhi na kwamba serikali haitakuwa tayari kumuongezea muda.

“Natoa agizo kwa mkandarasi anayetekeleza utandika wa mabomba na kazi nyingine kuukamilisha kwa wakati ….na pia wakandarasi wote nchini wanaotekeleza miradi ya maji kuhakikisha wanaongeza Kasi na ikamilike ili wananchi wanufaike,”alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dk. Anna Mgwihira, alisema mkandarasi huyo alianza kusuasusa katika mradi huo na kwamba uamuzi wa serikali ni mzuri na unalenga kuwasaidia wananchi.

Naye Mbunge wa Mwanga, (CCM), Joseph Tadayo amesema mkandarasi huyo alivunja mkataba mwenye na kuondoka katika eneo hilo na kwamba ni vema serikali ikaarakisha mchakato wa kumpata mkandarasi mwingine.

“Wananchi wameulinda huu mradi tulipiga kelele sana juu ya huyu mkandarasi lakini bahati nzuri amevunja mkataba mwenye,wafanyakazi walioachwa wasubiri na wavute subra wakati changamoto zao zikiendelea kutatuliwa,”alisema.

Katibu wa chama Cha mapinduzi mkoa was Kilimanjaro, Jonathan Mabihya,alitoa wito kwa serikali kutatua changamoto za ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya wilaya ya Same, Mwanga na Hai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles