Arodia Peter, Dodoma
Serikali imepiga marufuku wakuu wa vyuo vikuu nchini kuingilia chaguzi za wanafunzi vyuoni.
Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 30, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, wakati wakati akihitimisha na kujibu hoja za wabunge kuhusu suala hilo.
Amesema wanafunzi wanaruhusiwa kufanya siasa zao vyuoni na wasiingiliwe kwenye chaguzi zao.
” Serikali haijazuia siasa vyuoni isipokuwa kinachokatazwa ni siasa za vyama vya siasa,” amesema Ole Nasha.