25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mbatia: Wabunge tuache tofauti kuokoa elimu

Arodia Peter, Dodoma

Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi),  amewashauri wabunge kuondoa tofauti zao na kuhakikisha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatengewa fedha za kutosha ili kuokoa elimu ya Tanzania.

Mbatia ametoa ushauri huo wakati wa mjadala wa wizara hiyo bungeni leo Aprili 30, ambapo amesema sekta ya elimu inahitaji utulivu na kukubaliana kama taifa mustakabali wa kizazi hiki na kijacho.

“ Lazima  tuwaze kwa upana namna gani tunakuza watoto wetu, namna gani tunawapa uwezo walimu wetu ambao ni walezi wakuu wa taifa letu waweze kuliangalia taifa na kuwa watulivu.

“ Sasa hapa kila siku tunapiga kelele,  Naibu Waziri, Ole Nasha chonde chonde tuache tofauti zetu, tuwe na utulivu wa ndani, tuondoe tofauti zetu kutubaliane namna ya kulea watoto wetu,” amesema Mbatia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles