23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Makaramba astaafu

Na Happiness Katabazi

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ,Robert Makaramba amestaafu rasmi utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii jaji huyo amesema leo Aprili 30 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambapo ametimiza umri wa miaka 60 na miaka 33 ya utumishi wa umma.

Ibara ya 110 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema jaji wa Mahakama Kuu atastaafu akiwa na umri wa miaka 60.

Jaji Makaramba ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania tangu mwaka 1995 amesema anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kutimiza umri huo na kustaafu salama utumishi wa umma.

“Najisikia furaha isiyo na kifani baada ya kutumikia mhimili wa Mahakama hususani kuwasikiliza wananchi wanyonge waliokuwa wakifika mahakamani kutafuta haki bila ya kuwa na msaada wa kisheria, ” amesema Jaji Makaramba.

Jaji Makaramba ambaye aliteuliwa kuwa jaji mwaka 2006, miongoni mwa kesi maarufu alizowahi kusikiliza ni kesi ya uchaguzi No.20/2005 ya kupinga ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Dk.Wilbroad Slaa (CHADEMA), ambapo Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilimtangaza kuwa ndiyo mshindi .

Jaji huyo aliwahi pia kuwa mhadhiri katika Kitivo Cha Sheria katika Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kuanzia mwaka 1988-2003.

Aidha mwaka 2003 hadi 2006 alikuwa Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na wajumbe wa tume hiyo ndiyo walikuwa waanzilishi wake ambapo ilikuwa chini ya Mwenyekiti marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Dk. Robert Habesh Kissanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles