23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali: Fursa kuwavutia wawekezaji wa nje zipo

dk-ashatu-kijajiHERIETH FAUSTINE NA ESTHER MNYIKA – DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema licha ya kuwapo malalamiko katika uwekezaji wa huduma za fedha nchini, bado kuna fursa nzuri zinazowavutia wawekezaji kutoka mataifa tofauti.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya UBL, Kariakoo.

Alisema hivi karibuni kulikuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya taasisi za kifedha na kutoa viashiria vya kufilisika, lakini uzinduzi wa tawi hilo ni ishara tosha kuwa sekta ya uwekezaji wa huduma za kifedha bado ipo imara na itaendelea kuwavutia wawekezaji.

“Uchumi wa Tanzania kwa sasa unakua na Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya UBL imevutiwa na hali hiyo na kuamua kuwekeza nchini.

“Benki ya UBL Tanzania ilianza rasmi Septemba mwaka 2013 na kufanikiwa kupata faida iliyosababisha kuzindua tawi jingine, huku ikiwa na mipango ya kufungua matawi kadhaa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Arusha. Hii ni ishara tosha kuwa sekta ya huduma ya kifedha Tanzania inakua na kupata maendeleo makubwa,” alisema Dk. Kijaji.

Alisema kuwa benki hiyo kwa sasa imetumia zaidi ya Sh bilioni 67 kutoa mikopo kwa wateja wake na huduma nyingine.

Naye Rais na Mtendaji Mkuu wa UBL, Wajahat Husain, alisema kuwa wamefurahishwa na hali ya uwekezaji iliyopo nchini na kuamua kuwekeza.

Alisema wameichagua Tanzania kutokana na kukua kwa uchumi, hali bora ya kisiasa, maliasili na huduma za Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni kiungo cha wafanyabiashara, si kwa Tanzania tu, bali hata kwa nchi sita jirani.

Mtendaji huyo alisema kupanuka kwa mtandao wa benki hiyo kwa Dar es Salaam kutaifanya kuwa kiungo muhimu cha masuala ya kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles