24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ndassa aachiwa huru kesi ya rushwa

ndassaNa KULWA MZEE

  • DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuomba rushwa ya Sh milioni 30 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba, ameachiwa huru.

Ndassa (56) aliachiwa huru jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya Jamhuri kuwasilisha hati wakionyesha hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Mbunge huyo ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji, alipandishwa kizimbani Aprili mosi mwaka huu na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Dennis Lekayo,

Ilidaiwa katika hati ya mashtaka kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 13, 2016, jijini Dar es Salaam kinyume cha kifungu cha 15 (2) cha Sheria ya Takukuru.

Lekayo alidai kuwa katika shtaka la kwanza, siku hiyo ya tukio mshtakiwa kwa nafasi yake ya Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji, aliomba rushwa ya Sh milioni 30 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba.

Ilidaiwa mshtakiwa huyo alishawishi na kuomba rushwa hiyo ili kamati yake iweze kutoa hati safi ya ukaguzi wa ripoti ya hesabu za mwaka 2015/2016 kwa shirika hilo.

Katika shtaka la pili, Ndassa alidaiwa kumshawishi Mkurungezi Mkuu wa Tanesco, Mramba, kumpatia umeme ndugu yake aliyetambulika kwa jina la Matanga Mbushi na rafiki yake Lameck Mahewa, akimshinikiza atoe huduma hiyo ili kamati yake iweze kutoa hati safi ya ukaguzi wa ripoti ya hesabu ya mwaka 2015/2016 kwa shirika hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles