23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ujerumani yasaidia wakimbizi bilioni 26/-

egon-kochanke-and-magufuli1Na JOHANES RESPICHIUS- DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Ujerumani kupitia ubalozi wake hapa nchini, imetoa msaada wa Sh bilioni 26.4 kusaidia wakimbizi walioko katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kama vile Kigoma na Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke, alisema fedha hizo zitatengwa mara mbili. Kiasi kitapelekwa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) na nyingine Shirika la Chakula Duniani (WHO).

“Fedha hizi tumezitenga kwenye mafungu haya kwa sababu kila shirika moja lina majukumu yake kwa wakimbizi. Mfano WHO ni kwa ajili ya kuhudumia chakula na UNHCR inashughulikia mambo mengine kama afya na usalama,” alisema Kochanke.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba, alisema Tanzania kwa kushirikiana na nchi mbalimbali zinaendelea kushirikiana ili kuhakikisha wakimbizi wanapungua.

“Tunaendelea kutatua migogoro inayoendelea katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ili kuhakikisha suala la wakimbizi linapungua kwa kiasi, ndiyo maana Jumuiya ya Afrika Mashariki ilimteua Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, kwenda kupatanisha katika mgogoro wa Burundi.

“Naamini matumizi ya fedha hizi hayatakuwa na mwingilio wowote wa kisiasa au matumizi mengine nje ya lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wakimbizi,” alisema Balozi Simba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles