Na Mwandishi Wetu
KUNA picha mbaya inajengeka kati ya sekta binafsi na ile ya umma kuwa Utawala unaichukia sekta binafasi na hivyo haiishirikishi katika miradi yake mikubwa na kufanya biashara yenyewe pekee na hivyo kuwa shindani nayo hali amabayo inafifisha uchumi na hivyo kukuwa kwa kiwango kidogo kuliko ilivyotegemewa.
Hali hiyo kwa mtazamo huo potofu inasemekana imekuwa mbaya zaidi katika awamu ya tano ambayo imefanya mengi makubwa na kuiacha sekta binafsi katika hali ya sintofahamu na unyonge.
Rekodi mbaya ya utendaji kazi pamoja na historia ndefu ya matatizo kwa sekta binafsi katika miradi fulani ya maendeleo imesababisha serikali kuwekeza na kutekeleza yenyewe bila ubia na binafsi katika miradi ya miundombinu mikubwa ya reli ya viwango (SGR ) mradi wa umeme Stiegler na ule wa bomba la mafuta la Hoima hadi Tanga.
Serikali kupitia wazir wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati wa kujadili bajeti ya fedha ya 2018 ya 32.47trn / – na Mpango wa Taifa wa Maendeleo katika Bunge la Oktoba mwaka jana Waziri wa Fedha na Mipango, alisema na kusisitiza kuwa serikali itaendelea na kukopa kwa busara ili kufanikisha miradi yake ya maendeleo kama sekta binafsi haikutumia njia ya mwenendo wa rafiki anayehitaji kwani umfaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
“Sio kwamba serikali haitaki kushirikisha sekta binafsi katika miradi yake ya maendeleo; tunajua ni injini ya ukuaji wa uchumi, lakini tunauzoefu mbaya na ninyi nyote ni mashahidi, ” alisema Dr Mpango.
Ndio. Nani asiye jua IPTL na na TRL matatizo yaliyotokanayo na ushirika ambao uliishia kulana kisogo na kuliingiza taifa katika migogoro isiyoisha ya nishati na miundombinu ya ya reli na mgawo wa umeme? Vipi ushirika wa TTCL na utapeli uliofanywa kwa Shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) na TBC ushirika wake na Star Media?
Alisema serikali itaendelea kukopa madeni ya muda mrefu kama madeni ya kitaifa ili kuboresha uwezo wa uchumi wa ndani na kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo muhimu kwa riba kwani ni muhimu kufanya hivyo kwa manufaa ya wote.
Waziri Dk Mpango alisema serikali itatumia rasilimali zake yenyewe kwa ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli ya kiwango cha wastani (SGR) pamoja na mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge, bila kusahau kurekebisha viwanja vyake vya ndege vilivyo katika hali mbaya na kukosa huduma muhimu pamoja na uchakavu wa miundombinu.
“Ninyi nyote mnajua kile kilichotokea hadi tulipaswa kuingiliana na kile ambacho faragha na vidokezo vya faragha vilifanywa kwa Shirika la Reli la Tanzania, Kampuni ya Mawasiliano ya Tanzania na Air Tanzania ili kutaja machache,” alisema.
Aidha, alisemaDk Mpango kuwa sekta binafsi haijakuja wakati inapohitajika ila kwa wakati wake wenyewe na kufanya hivyo, huweka meza kwenye hali ngumu na kufanya serikali ijisikie unyonge na kutoa maamuzi ya kufanana na viatu vyake na hivyo kuendesha miradi hiyo pekee kwani ni wajibu wake kufanya hivyo.
Alisema changamoto hizo zinazoletwa na sekta binafsi zilifanya serikali kuzingatia uwezekano wa kuendesha baadhi ya miradi yake, ambayo alisema kuwa na matokeo mazuri, akisema kuwa katika zaidi ya miaka kumi, serikali imewekwa kupata mgawanyo wa 1bn / – kutoka TTCL. Ni kweli na haki ?
Dr Mpango alisema wanathamini Ubia wa Umma na Binafsi (PPP) au P3 na kila wakati kuna fursa, watafanya hivyo kulingana na sifa ya mradi kwa maslahi ya kitaifa.
Ni ukweli usiopingika kuwa Uzalendo mara nyingi umekosekana na watu kuweka sana mbele faida binafsi na ikiwezekana hata kufisidi kwani misingi yao ya maisha ni ile zaidi ya mwananchi wa kawaida.
“Tunathamini sekta binafsi, lakini wanapaswa kupimwa kwa nia na kujitolea kwao; serikali imekuwa huko, lakini changamoto ambazo tumekutana nazo, zimefanya sisi kufikiri mara mbili,” alisema Dk Mpango.
Alisema katika bajeti ya pili ya maendeleo ya kitaifa inayokuja mtazamo utakuwa katika sekta ya kilimo, upatikanaji wa maji ya kuaminika na kugusa fursa za rasilimali za gesi, kwa sasa ni lengo la uchumi wa viwanda.
Waziri Dk Mpango alisema kuwa Serikali itasimamia pia idadi ya ongezeko la watu ambao kwa sasa ongezeko lake ni asilimia 3.8 ambayo ni kubwa pamoja na kuboresha uchumi wa Taifa unaokua kwa asilimia 7 ili uwe zaidi ya asilimia 8 ili nchi iweze kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.
Alilithibitishia Bunge la Taifa kwamba atafanya kazi kwa mapendekezo yake ili aweze kurekebisha Mpango wa Taifa wa Maendeleo mwaka ujao, ambao anaona utakuwa na maoni yao mengi.
Wabunge waliwasilisha hisia za wafanyabiashara nchini ambao walilaumu serikali kwa kutowahusisha kwenye miradi mikubwa na hivyo kushindana nayo katika kukopa katika mabenki ya ndani na kufanya kiwango cha riba kupanda.
Kwa mtazamo wao ni kuwa serikali ikope nje na wao wakope ndani na hivyo utapatikana urari murua wa mikopo kwani mabenki hupendelea amana za serikali na hatifungani zake kuliko mikopo ya wafanyabiashara ambayo haina uhakika.
Kwa mwaka jana mikopo chechefu ilikuwa mingi kuliko kwa kufikia kiwango cha asilimia zaidi ya 9.5 ikiwa mara mbili ya kiasi kilichozoeleka na hivyo kufanya mabenki kutishika kukopesha kwa watu binafsi au kuweka masharti magumu ya mikopo licha ya Benki Kuu kupunguza viwango na vigezo vya mikopo inayotolewa.
Historia ya hivi karibuni imeonyesha kuwa moja ya changamoto kubwa zaidi kwa miradi ya P3 ni ile ya kisiasa, kwa mujibu wa miradi iliyopendekezwa kupata kukubalika kwa kutosha ndani ya wakazi wa eneo hilo. Kutokana na historia hii – na kama hatupendi taifa letu la mamilioni ya kushikilia P3s nyuma – basi ushirikiano na kampuni inayofaa kufaa inaweza kusaidia.Hasa, makampuni yenye mizizi yenye nguvu ya ndani huelewa zaidi mienendo ya siasa na jamii ambayo ni muhimu kwa kukubali na kufanikiwa kwa miradi ya P3.