22.1 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Sean atemana na Kanye

LOS ANGELES, Marekani

IKIWA ni miaka minne tangu aliposajiliwa, rapa Big Sean ametangaza kuachana na lebo ya G.O.O.D. Music inayomilikiwa na staa wa muziki, Kanye West.

Akiwaambia mashabiki wake kupitia ukurasa wa Twitter jana, Sean amesema uamuzi huo haujatokana na ugomvi, bali ni katika kujitanua zaidi kimuziki.

Akiwa na G.O.O.D. Music, alifanya vizuri sokoni, ikiwamo albamu yake ya ‘Detroit 2’, na sasa ataendelea kufanya kazi na lebo nyingine kubwa, Def Jam Recordings.

Tayari ameshaachia ‘EP’inayokwenda kwa jina la ‘What You Expect’ikiwa na ngoma sita, ambayo prodyuza wake ni Hit-Boy ambaye ndiye aliyesimamia albamu yake kali ya ‘Detroit 2’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles