24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Buhari awaonya wanaotaka ang’ang’anie Ikulu

MAKKAH, Saudi Arabia

AKIZUNGUMZA na raia wa Nigeria wanaoishi mjini Makkah, Rais Muhammadu Buhari amewaonya wanaoendesha kampeni za kumtaka aongeze muda wa kubaki madarakani.

Rais Buhari aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2015, anaelekea ukingoni mwa awamu yake ya pili na amesema ameshaapa kwa Mungu kwamba ataondoka Ikulu mwaka 2023.

“Niliapa kwa Qur’an Tukufu kwamba ningeongoza kwa mujibu wa Katiba na kisha kuachia madaraka muda unapofika. Hakuna nyongeza ya utawala. Sitaki yeyote azungumzie hilo na kuendesha kampeni za kuongeza muda wa utawala kinyume cha Katiba. Sitakubali,” amesisitiza.

Aidha, aliwaomba Wanigeria kuacha utamaduni wa kukosoa kila kinachofanywa na Serikali yake, wakisahau kuwa yapo mazuri, ikiwamo namna ilivyoshughulikia amani maeneo ya Kaskazini-Mashariki mwa taifa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles