28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani: Virusi vya Corona havijatengenezwa

NEW YORK, Marekani

MAOFISA wa usalama nchini Marekani wamesema huenda isiwezekane kujua chanzo cha Corona lakini si kweli kwamba virusi vya ugonjwa huo vilitengenezwa kwa lengo la kutumika kama silaha.

Tangu kuibuka kwa janga hilo ulimwenguni, China imekuwa ikinyooshewa vidole kwamba ndiko lilikotokea lakini Ofisi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa nchi hiyo (ODNI) imekuja na mtazama tofauti.

Katika ripoti hiyo ambayo ni maboresho ya ile ya Rais Joe Biden ya miezi miwili iliyopita, ODNI imesema bado imebaki kuwa ni hisia tu na hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuthibitisha hilo.

Aidha, ripoti hiyo pia imewatoa lawamani viongozi wa China ikisema hawakufahamu lolote juu ya uwepo wa virusi vya Corona hadi pale ugonjwa ulipoibuka katika Mji wa Wuhan mwishoni mwa mwaka juzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles