29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

SBC yakabidhi 50m/- kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera

majaliwaKampuni ya SBC Tanzania Limited,watengenzaji wa vinywaji baridi (Pepsi), imemkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kiasi cha Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu.

Tetemeko hilo liliua watu wapatao 16, kujeruhi wengine zaidi ya 200 huku likiacha mamia wakiwa hawana malazi, chakula na huduma nyingine za kijamii.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa SBC Tanzania Limited (Pepsi), Avinash Jha amesema kampuni yake imeguswa na janga hilo la kitaifa na linaungana na wadau wengine kuchangia msaada kwa waathirika hao.

“Tunaunga mkono jitihada za Serikali na Mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli  kusaidia waliopatwa na janga hili. Tupo pamoja ili kuwafariji walioopoteza ndugu, jamaa  au rafiki ikiwamo na kuharibikiwa kwa makazi, miundo na kusabisha wamia ya watu kukosa huduma za msingi za kijamii,” alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Akitoa mifano ya misaada iliyotolewa na SBC, Mkurugenzi Jha amesema mwaka huu pekee wameshazawadia madawati zaidi ya 200 kwa shule ya msingi mkoani Dar es Salaam na kupitia ofisi ya mkoa wa Shinyanga wametoa Shilingi milioni 20 ili kutatua changamoto la madawati kwa wanafunzi wa shule.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu  Mhe. Kassim Majaliwa alishukuru uongozi  wa kampuni hiyo na kusema kuwa msaada huo umefika wakati mwafaka kwani wakazi wa mkoa wa Kagera wanahitaji msaada wa kukarabati na kujenga makazi na miundo mbinu zingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles