27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Saudi yamfukuza balozi Lebanon

RIYADH, Saudi Arabia

SAUDI Arabia imetoa agizo la kumtaka balozi wa Lebanon nchini humo kuondoka ndani ya saa 48 kwa kile ilichoeleza kuwa ni ‘matusi’ ya Serikali yake.

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Habari wa Lebanon, George Kordahi, kukosoa hatua ya Saudi na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kupeleka majeshi katika nchi ya Yemen.

Kwa miaka saba sasa, Yemen imekuwa kwenye vita, ambapo majeshi yanayoongozwa na Saudi yamekita kambi yakipambana na Kundi la waasi la Houthi.

Katika kauli yake ya kuzikosoa Saudi na UAE, Kordahi aliwatetea wanamgambo wa Houthis akisema wanachofanya ni kujilinda dhidi ya udhalimu wa mataifa hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles