23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Samwel Sitta aliandika historia bungeni

samwel-sittaOktoba 2, 2014, Samuel Sitta aliandika historia yake mpya kwa kuliongoza Bunge Maalumu la Katiba kupitisha rasimu ya Katiba iliyopendekezwa.

Rasimu hiyo ilifanikiwa kupita baada ya kura za ndio zilizopigwa na wajumbe kufikia kiwango kinachostahili, huku ikisusiwa na wajumbe wa bunge hilo waliounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Upigaji kura ambao ulianza Septemba 29 hadi Oktoba 2, siku matokeo yalipotangazwa, ulisusiwa na wabunge wengi wa upinzani, kwa madai kuwa baadhi ya vipengele vya awali vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi vilikuwa vimeondolewa.

Kabla ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, Bunge hilo maalumu la Katiba lilikaa kama kamati kujadili mapendekezo katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na tume hiyo ya mabadiliko ya katiba iliyokuwa chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles