30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Apumzike Sitta, alifanya mengi kwa miaka 74

sitta-1ALIYEKUWA Mbunge wa Urambo kwa miaka 40  (1975 hadi 2015), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa miaka mitano (2205 hadi 2010) na Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefariki dunia jana.

Alizaliwa mwaka Desemba 18, 1942 na amefariki dunia jana Novemba 7 (2016) akiwa na miaka 74.

Sitta alilitumikia Taifa hili katika nafasi mbalimbali tangu akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi serikalini, ikiwamo uwaziri na uspika wa Bunge.

Alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) kwa miaka tisa tangu 1996 hadi 2005; na kuwa Spika wa Bunge baada ya kuchukua nafasi ya Pius Msekwa aliyekuwa Spika wa Bunge hilo kwa miaka kadhaa.

Sitta alifanya kazi ya uspika tangu Desenba 26, 2005 hadi Julai 10, 2010 ambapo alisifika kuwa spika wa kasi na viwango. Akiwa Spika, alisifiwa pia na wapinzani kwa kutopendelea chama chake bali haki ilitawala wakati akiliongoza Bunge.

Novemba 28, 2010 aliteliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki hadi Januari 24, 2015 wakati nafasi hiyo ilipochukuliwa na Harrison Mwakyembe.

Januari 24, 2015 aliteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi hadi Novemba 2015 ambako, katika kipindi hicho, alifanya mabadiliko ya uongozi katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuipa msukumo wa ufanyaji kazi wa kutumainiwa.

Ni vigumu sana kueleza kwa kina mchango wa Sitta katika kulitumikia Taifa hili na kusukuma maendeleo yake. Alikuwa mwepesi na mchangamfu kutumikia popote.

Aliwania kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba na kufanikiwa hadi Katiba Inayopendekezwa ikapatikana baada ya mshikemshike na mvutano mkubwa uliokuwa unatokea wakati wa vikao vya Bunge, hasa miongoni mwa wabunge wa chama tawala (CCM) na Upinzani.

Aliweza hata kusimama kidete wakati siku chache baada ya Jukwaa la Kikristo Tanzania kutoa waraka wa kupinga mchakato wa Bunge Maalumu la Katiba, (Sitta) aliuponda waraka huo na kudai kuwa ulikuwa umetengenezwa kisiasa kwa kuwaunga mkono wajumbe wa Ukawa waliokuwa wamesusa Bunge hilo.

Waraka huo ambao ulitolewa na jukwaa hilo lililokuwa limeundwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Wasabato (SDA) na Jumuiya ya Kikristo (CCT), lilisema Bunge hilo lilikuwa likiendesha vikao vyake huku likiwapotosha wananchi kwa makusudi.

Sitta alisema kuwa maaskofu hao wangekuwa na matendo mema walipaswa kuwa wa kwanza kutangaza amani nchini, lakini walikuwa mstari wa mbele kuingilia masuala ya kisiasa ambayo yalikuwa yanakwenda kinyume cha maadili ya kazi yao.

Kwamba hayo yalikuwa si mambo ya kiroho kwa sababu yalikuwa yanamwambia Rais asimamishe mchakato huo ili kupisha maridhiano na mwafaka.

Sitta alisema yeye akiwa kiongozi lazima alipaswa kuonyesha kukataa hali hii kwa sababu waraka kama huu ungeruhusiwa kusomwa makanisani ungeweza kupeleka nchi pabaya.

Sitta ana mambo lukuki aliyoyafanyia nchi hii, ni mengi kuweza kuyaorodhesha.

Tunasema inatosha tu Mungu amependa kumchukua, ampumuzishe kwa amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles