26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Salma Kikwete ataja vipaumbele sita vya Jimbo la Mchinga

Mwandishi Wetu, Lindi

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mchinga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Salma Kikwete, ametaja vipaumbele sita atakavyovisimamia na kuvitekeleza endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Salma ambaye pia ni mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, amevitaja vipaumbele hivyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo lililopo mkoani Lindi kuwa ni elimu, afya, maji, miundombinu, nishati na michezo.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Uwanja wa Mchinga Moja jana na kuzinduliwa na Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa pia na Kikwete, viongozi wa Serikali na CCM wa Mkoa na Wilaya ya Lindi, Salma, alisema akichaguliwa atashirikiana na Serikali kuhakikisha matatizo yote ya jimbo hilo yanatatuliwa na atasimamia vipaumbele vyake alivyovitaja.

“Sababu na nia ya kugombea ni msukumo wa wana Mchinga walioniomba nigombee jimbo hili, kila kata niliyotembelea na maeneo niliyotembelea waliniomba nigombee na wengine kikundi cha watu walienda kwa Kikwete kupeleka ushawishi wa kutaka nigombee, kwanza nilikataa, nikakataa lakini baadaye nikakubali kwa ajili ya kutaka kuleta maendeleo ya Mchinga, alisema Salma na kuongeza:

“Malengo yangu ya baadaye ni nini, nitafanya nini, nitakayoyafanya ni nini na nitakayoyasimamia ni nini? Vipaumbele vyangu ni elimu, afya, mundombinu, maji, nishati na michezo. Nini nitafanya mwaka 2020 na mwaka 2025 mkinichagua kuwa mwakilishi wenu wa Mchinga? Mkinichagua nitashirikiana na Serikali kuhakikisha tunakuwa na shule ya sekondari ya kidato cha tano na sita hapa Mchinga.

“Nitalisimamia hili bega kwa bega na ushahidi mmeuona hapa Mama Samia amekuja Mchinga, mkinichagua nitakwenda kwa Mama Samia moja kwa moja na kumweleza matatizo ya Mchinga hasa katika maeneo yote ambayo nimeyataja, kwa kushirikiana na Serikali nitaboresha elimu ya sekondari kwa kuboresha madarasa, nyumba za walimu na kukamilisha maabara zote ambazo hazijafikia kiwango kinachostahili.”

Kuhusu mafanikio ya elimu bila malipo iliyotolewa na Serikali ya Rais Dk. John Magufuli kwa Jimbo la Mchinga, Salma, alisema Sh bilioni 1.099 zilitolewa huku idadi ya wanafunzi ikiongezeka kutoka 40,760 mwaka 2015 hadi kufikia 46,348 mwaka 2020 pia madarasa 80 yamejengwa, matundu 78 ya vyoo yamejengwa na vyumba tisa vya walimu vimejengwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles