23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi wa Makumbusho wazingirwa na majitaka kwa miezi minne sasa

Na MWANDISHI WETU

WAKAZI wa eneo la Makumbusho Mtaa wa kijitonyama Bwawani, wamelalamikia kuzingirwa na majitaka yenye kinyesi kwa zaidi ya miezi minne, huku mamlaka zinazohusika zikiwa hazijachukua hatua yoyote ya wazi.

Wakizungumza na MTANZANIA jana, baadhi ya wananchi wa mitaa ya Tanzania, Mali na Soweto katika eneo la Makumbusho walisema wamekuwa wakiishi kwa kuzingirwa na majitaka hayo kwa muda wote, kutokana na kuharibika kwa mfumo wa majitaka wa eneo hilo.

Mmoja wa wakazi hao ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa ujenziw a mfumo wa majitaka mwaka 1998, Dennis Kessy alisema hali hiyo imekuwa kero, kutokana na mfumo wa majitaka uliopo kuzidiwa na kuharibika hivyo maji kurudi kwenye makazi ya watu.

Aliema mfumo wa majitaka kwenye eneo hilo ulikuwa maalumu kwa ajili ya makazi ya watu wa zilizokuwa nyumba za Shirika la Nyumba la taifa (NHC) ambao walichangia Sh. 90000 kila nyumba kwa ajili ya jenzi wa mfumo huo mwaka 1998, ambao kwa sasa umeidiwa kutokana na ongezeko la majengo.

“Kama unavyoona, wakati mfumo huo unajengwa na wananchi kwa kushirikiana na Irish Aid hakukuwa na maghorofa, lakini sasa hivi kuna maghorofa yamefumuka kama uyoga kwenye eneo la makazi na wote wanategemea mfumo huo huo ambao ulitengenezwa kuhudumia watu wachache.

“Mfumo huo ulikuwa maalumu kw aajili ya kupokea maji machafu kutoka kwenye makazi yetu na kuyapeleka moja kwa moja baharini kwa hiyo sisi hatukulazimika kujenga makaro. Lakini zaidi mabomba yaliyotumika yalikuwa yenye uwezo wa kubeba mzigo wa wakati ule, ambayo yalikuwa ni ya inchi sita kwenye bomba kuu na ya kutoka kwenye nyumba yalikuwa ya inchi nne, sasa hivi yamezidiwa, yamepasuka na chemba zinatema maji yanaishia kufurikakwenye makazi,” alisema Kessy.

Alisema kwamizi mitano sasa tangu mfumo huo wamajitaka ulipoharibika maji hayo yenye vinyesi yamekuwa yakitapakaa kwenye makazi ya watu na hata baada ya kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika, ikiwemo Mamlaka ya Majisafi na Maji Taka ya Jiji la Dar es Salaam (Dawasa) hakuna hatua zoote zilizochukuliwa.

Alisema kwa sasa hawana namna ya kufanya kwa kuwa hawana ameneo ya kujenga makaro na mara nyingi uchafu wa vinyesi umekuwa ukufurika ndani ya nyumba zao, hivyo kuiomba Serikali ya mkoa iwasaidie kuondokana na hali hiyo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Angela Mganga alisema ameishi hapo kwa miaka 46 sasa lakini hajawahi kushuhudia kero ya aina hiyo, ambayo imemlazimisha kuhamaisha watoto wake na kuwapeleka kwa ndugu zake. 

Alisema nyumba yake iliyoko kwenye Mtaa wa Tanzania ni miongoni mwa nyumba ambazo maji yenye kinyesi yamekuwa yakiizingira muda wote kwa zaidi ya miezi minne sasa huku akiwa hajui la kufanya.

“Tumechukua hatua, tumekwenda serikali ya mtaa kuomba msaada, tumekwenda hadi kwa Dawasa wilaya pale mwano tu tatizo hili lilipoanza, walikuja wakachukua picha wakaondoka. Hkuna hatua yoyote miezi minne sasa,” alisema.

Mganga alisema nyumba yake na nyumba za majirani zake wawili wanaomzunguka ni miongonbi mwa zilizoathirika ambazo zimezingirwa na majitaka yenye vinyesi kwa zaidi ya miezi minne sasa.

“Tumelaalmika mara kadhaa,kwa vuiongozi wa Serikali, Dawasa lakini tunachoona ni kwamba hakuna anayejali, labda kwa kuwa tatizo hili haliko kwao,” alisema.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama Bwawani, Felicianus Kamukara alisema kwa upande wake amajaribu kuchukua hatua kadhaa ikiwemo za kuwasiliana na mamlaka husika ikiwemo Dawasa, kwa kuwa tatizo hilo lipo katika eneo kubwa kwenye Kata ya Kijitonyama lakini anashangazwa na ukimya uliopo.

Alisema kwa maelezo ya wataalamu alijaribu kuzunguma nao ni kwamba tatizo lipo kwenye makutano ya barabara ya Sayansi ambapo eneo hilo linadaiwa kutitia hivyo kuathiri mfumo wa mabomba ya majitaka yanayokwenda kumwaga maji hayo baharini.

“Lakini ni kweli kwamba tatizo hili ni kubw akwa wakazi wa eneo hili, ni karibu miezi mitano sasa haya majitaka yenye vinyesi hayaendi popote, yametuama katika maeneo ya makazi. Nimejaribu kuchukua hatua hata kufika kwa Mkuu wa Wilaya lakini bado tatizo hili halijapatiwa ufumbuzi,” alisema Kamukara.

Ofisa Habari wa Dawasa, Evalasting Lyaro alisema ofisi yake haina taarifa za tatizo hilo lakini hata hivyo atafuatilia ili kujua undani wake.

“Kwa kweli ofisi yangu haina taarifa kuhusu tatizo hilo, ila nashukuru kw akunifahamisha. Ninaomba unitumie majina ya hayo maeneo kwenye meseji (ujumbe mfupi wa maneno) ili nifuatilie kwa anayehusika na masuala ya majitaka kujua tatizo ni nini,” alisema Lyaro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles