24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

SALAMU ZA WARUNDI BONGO MUVI  

BONGO MUVINA KYALAA SEHEYE HANCHA

STAA wa filamu nchini Burundi, Lydia Keisha Ndayiziga amesema Warundi wanavutiwa sana na sinema za Kibongo na kwamba soko lake ni kubwa  nchini humo.

Akipiga stori na Swaggaz, juzi jijini Dar es Salaam, msanii huyo alisema hata yeye alijikuta akishawishika zaidi kuingia kwenye uigizaji baada ya kuona kazi nzuri za Watanzania akiwa nyumbani kwao huko Bujumbura, Burundi.

“Soko la filamu za Kibongo Burundi ni kubwa sana. Nakumbuka hata mimi nilianza kuvutika zaidi na filamu za Kibongo. Niliona sinema moja amecheza Kanumba (marehemu), nikasisimka sana, nikaona kumbe natakiwa kuwa mwigizaji,” alisema Ndayiziga.

Anasema, tangu hapo aliamua kuachana na ndoto zake za kusomea Kozi ya Human Resource Management akiwa na lengo la kutetea haki za binadamu nchini mwake, akaamua kuituliza akili yake kwenye filamu ili aelimishe kupitia upande huo.

“Nashukuru Mungu kuona ndoto zangu zimetimia. Kule nyumbani nimecheza sinema nyingi lakini Niyonsavye na Mapenzi ya Kweli ndizo zilizonipa umaarufu zaidi.

“Lakini ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kuja kucheza sinema hapa Tanzania. Nimefurahi sana kupata connection na mwigizaji Shamsa Ford ambaye tayari nimeshacheza naye sinema iitwayo Najuta Shamsa,” alisema.

Amesema mbali na sinema hiyo aliyocheza na Shamsa, amecheza muvi nyingine inayokwenda kwa jina la Duma Smart Boy huku kwa sasa akiwa location akirekodi kazi nyingine ambayo hajaitaja jina lake.

“Najisikia vizuri kuona ndoto zangu zinatimia. Nilitamani sana kuja kucheza sinema na wasanii wa Bongo Muvi, naona kabisa njia zangu za mafanikio kimataifa zikiachia,” alisema Ndayiziga.

Mbali na Ndayiziga, baadhi ya wasanii wengine kutoka nje ya Tanzania waliokuja nchini kushiriki filamu na mastaa wa Bongo ni Nkiru Silvanus, Femi Ogadegbe, Emmanuel Francis, Mercy Johnson, Bimbo Akintola na Ramsey Noah (Nigeria) waliocheza sinema mbalimbali na marehemu Steven Kanumba.

Wengine ni Mzambia Cassie Kabwita aliyecheza sinema kadhaa na Jacob Stephen ‘JB’ na Mghana Van Vicker aliyekuja nchini kwa mwaliko wa Hashim Kambi na kushiriki Filamu ya Never Give Up.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles