Mjumbe wa Serikali ya kijiji, Salum Ikanda anasema sasa ni tafrani na amani ni ndogo kijijini hapo.
Watu wamekimbia maporini kujihami, walosalia majumbani ni wanawake tu.
Gari mbili za polisi zafika kijiji na kuanza kukamata watu.
Hadi sasa watu takriban 30 wamekwisha kamatwa na polisi na kati yao kuna viongozi wa kijiji wanne wakiwemo Diwani Kata ya Jangalo-Seraji Lubuva, Mwenyekiti wa Kijiji-Bashiru Kilasi, Mwenyekiti Mradi wa Maji-Ibrahim Jororo na Mtendaji wa Kijiji- Muhammed Chobu
Kutokana na hali ilivyo sasa, Ikanda anasema kama Baraza la kijiji hawajui chakufanya kwani hawezi hata kukutana, hii ikiwa na maana watu wametawanyika wamekimbia makazi yao.