23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ruwasa Musoma waiandikia barua TANROADS

Na Shomari Binda, Musoma

WAKALA wa Maji Vijijini( Ruwasa) Wilaya ya Musoma, imesema miradi mbalimbali inaendelea kuhakikisha wananchi wanapata maji, huku ikiiandikia barua TANROADS kutokana na changamoto za kupitisha mabomba katika baadhi ya maeneo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Kijiji cha Wanyere Kata ya Suguti, Meneja wa Ruwasa,Edward Sironga,amesema yapo maeneo ambayo mabomba yanapita barabarani na tayari wamewasiliana na TANROADS ili kukamilisha miradi hiyo.

Amesema Kata ya Suguti kuna mradi wa maji wa kuwafikishia wananchi majumbani lakini bado baadhi  maeneo  hajafikiwa kutokana na changamoto ya kupitisha mabomba  barabarani.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, tumepewa zaidi ya bilioni nane kutekeleza miradi ya maji.

‘Tunamshukuru pia Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwa jitihada zake za kuwafikishia wananchi huduma,”amesema Sironga.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Suguti  wameshukuru kwa kufikishiwa huduma ya maji wakati kipindi cha nyuma waliyafuata zaidi ya kilometa 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles