24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Conte atua Tottenham

KLABU ya Tottenham Hotspur inayoshiriki Ligi Kuu ya England, imemtambulisha rasmi leo Novemba 2, 2021 Antonio Conte kuwa kocha mkuu wa timu hiyo hadi mwaka 2023.

Conte raia wa Italia anachukua mikoba ya Mreno  Nuno Espirito Santo aliyeachishwa kazi Jumatatu  kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho ikiwamo kipigo cha mabao 3-0 nyumbani  kutoka kwa Manchester United,  Jumamosi  Oktoba 30,2021.

Kupitia mitandao yao, klabu ya Tottenham imethibitisha kuwa kuanzia sasa Conte ndiye atakayekinoa kikosi hicho hadi 2023, huku kukiwa na makubaliano ya kuongeza mkataba huo.

“Tunayo furaha kutangaza kuteuliwa kwa Antonio Conte kuwa kocha wetu mkuu kwa mkataba unafikia ukingoni msimu wa joto wa 2023 na  kuna makubaliano ya kuongeza,” imesema klabu hiyo.

Conte alikuwa bado hajajiunga na klabu yoyote tangu alipoondoka Inter Milan katika majira ya joto, huku akikataa ofa mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles