33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

ROSTAND AIBEBA YANGA FA

Na MWANDISHI WETU -MBEYA

KIPA wa Yanga, Youthe Rostand, ameiwezesha timu yake kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), baada ya kuifunga Ihefu kwa penalti 4-3 katika mchezo wa hatua ya 32 bora uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya jana.

Mikwaju hiyo ya penalti ilitokana na timu hizo kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo.

Kipa huyo raia wa Cameroon, aliweza kupangua penalti mbili kati ya penalti sita na hivyo kuiwezesha timu hiyo kusonga mbele kwenye hatua ya 16 bora.

Katika mchezo huo, Ihefu itajilaumu kwa kushindwa kulinda bao lake walilolipata katika dakika ya 39, baada ya beki wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’, kujifunga wakati wa kuokoa hatari langoni mwake.

Ihefu wakiamini kuwa wameshinda mchezo huo kutokana na mwamuzi wa mchezo huo, Athumani Lazi, kutoka Morogoro kuongeza dakika sita, ziliwawaongezea nguvu Yanga na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 93 kupitia kwa Obrey Chirwa, baada ya kuangushwa katika eneo la hatari na beki wa Ihefu.

Katika mchezo huo, Yanga waliingia uwanjani wakiwa na matumaini ya ushindi tofauti na wapinzani wao.

Ihefu walionekana kutawala mchezo huo katika kipindi cha kwanza ambapo katika dakika ya tatu, mchezaji Joseph Kinyozi alikosa bao baada ya kupiga shuti akiwa katikati ya uwanja lililopaa juu.

Yanga nao walijibu mashambulizi katika dakika 18, ambapo Obrey Chirwa alikosa bao baada ya kupiga shuti na kudakwa na kipa wa Ihefu, Andrew Kayuni.

Inaendelea……………… kwa maelezo zaidi pata nakala yako gazeti la MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles