27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Rooney aomba radhi kuenea picha zake za ulevi

wayne-rooney-england-norway_3199516LONDON, ENGLAND

NAHODHA wa timu ya taifa ya England, Wayne Rooney, ameomba radhi baada ya kuenea kwa picha zake zinazomuonesha akiwa amelewa pombe mwishoni mwa wiki iliyopita.

Nyota huyo aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England na kocha wake, Gareth Southgate, kwa ajili ya mchezo dhidi ya Hispania ambao ulimalizika kwa sare ya 2-2, lakini mchezaji huyo hakupewa nafasi ya kucheza kutokana na kusumbuliwa na goti.

Kutokana na hali hiyo, kocha huyo alimruhusu mchezaji huyo kupumzika na nafasi ya kurudi katika klabu yake, lakini inadaiwa mchezaji huyo alionekana kwenye sherehe ya harusi katika hoteli ambayo timu hiyo ilikuwa inakaa wakicheza mechi ya kimataifa.

Inadaiwa kwamba Rooney mwenye umri wa miaka 31, alionekana akiwa amelewa na akiwa amevaa shati lenye nembo ya timu ya taifa ya Three Lions.

Gazeti la The Sun lilikuwa la kwanza kueneza picha za mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa klabu ya Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu nchini England.

Rooney amekiri kuwa amefanya makosa na picha hizo hazikutakiwa kusambaa kutokana na levo yake katika soka, kwa kuwa wachezaji wengi wanatamani kufanya kama aliyoyafanya yeye katika maisha ya soka.

“Picha zilizosambaa ni wazi kwamba hazifai kabisa kuonekana hasa kutokana na hadhi yangu, najua ni kosa ambalo nimelifanya, hivyo ni vizuri nikatumia nafasi hii kuwaomba radhi wachezaji wenzangu wa timu ya taifa, kocha wangu pamoja na mashabiki wote.

“Najua wengi wanatamani kufanya mambo kama ambayo nimeyafanya katika soka, sasa mambo kama haya yanaweza kushusha hadhi ya mchezaji pamoja na soka kwa ujumla.

“Haukuwa wakati sahihi wa mimi kufanya hivyo, kwa kuwa timu yangu ilikuwa katika michezo ya kimataifa, ninaamini jambo kama hilo haliwezi kurudia tena,” alisema Rooney.

Chama cha Soka cha England (FA) kimesema kitatathmini upya sheria kuhusu mambo ambayo wachezaji wanaruhusiwa kufanya wakati wao wa kupumzika.

Gazeti la The Sun linadai kuwa FA inataka kuchukua hatua hiyo kwa sababu wachezaji 10 wa timu hiyo ya taifa walikutwa Club usiku wa manane siku ya Jumapili, hivyo inaweza kuhatarisha maendeleo ya timu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles