24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mbarawa asainisha Bodi ya TRL

profesa-makame-mbarawaPATRICIA KIMELEMETA NA GRACE SHITUNDU-Dar es Salaam

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amezindua Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), huku akiwasainisha fomu ya kuwapima uwajibikaji (performance appraisal) ili atakayeshindwa kutimiza majukumu yake aondolewe.

Profesa Mbarawa alisema Dar es Salaam jana kuwa lengo la kuwasainisha katika fomu hiyo maalumu ni kuhakikisha   kila mmoja anawajibika kulingana na nafasi yake, hivyo basi wafanyakazi wavivu hawana nafasi ya kubaki kwenye shirika hilo.

Alisema Serikali haitawavumilia wafanyakazi wavivu watakaoshindwa kwenda na kasi ya uwajibikaji.

Alisema wafanyakazi wote wakiwamo wajumbe wa bodi, watajaza fomu hiyo kulingana na nafasi zao kazini ili kila mmoja aweze kuweka malengo   kwamba, ndani ya mwaka mmoja amewajibika kiasi gani, jambo ambalo linaweza kulisaidia shirika hilo  kujiendesha kwa faida.

“Kwa mara ya kwanza, wizara yangu imeanza kuwapa wafanyakazi fomu ya ‘performance appraisal’ ili tuweze kuwapima uwajibikaji wao, mtu anayeshindwa kufanya hivyo, namwondoa… nakufukuza kazi mara moja,” alisema Mbarawa.

Alisema lengo ni kuhakikisha shirika linajiendesha kwa biashara na kupata faida, jambo ambalo linaweza kusaidia kukuza uchumi.

“Katika kipindi hiki cha ushindani wa biashara, TRL inapaswa kutafuta masoko ya uhakika kwa wateja wa kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi ili kuongeza mapato,” alisema.

Alisema bila kufanya hivyo shirika hilo litaendelea kupata hasara siku hadi siku, jambo ambalo linaweza kusababisha Serikali kupata hasara na kuingia gharama kubwa ya kulipa madeni.

Msajili Hazina, Ephraem Mafuru, alisema wajumbe wa bodi wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano, kuongeza ufanisi kwenye kazi, jambo ambalo linaweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles