LISBON, URENO
MSHAMBULIAJI hatari wa timu ya taifa Ureno, Cristiano Ronaldo na beki wa kati wa timu ya Hispania, Sergio Ramos, wameweka tofauti zao pembeni mara baada ya mchezo wao wa kirafiki kati ya Ureno ambao walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya Hispania.
Baada ya kuwa marafiki kwa kipindi cha miaka tisa ndani ya klabu ya Real Madrid, wawili hao urafiki wao ulisimama kwa kipindi cha miaka miwili.
Moja ya sababu ambayo inatajwa kuwasababisha kutofautiana ni mara baada ya kiungo wa Real Madrid, Luka Modric kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa duniani ya Ballon d’Or dhidi ya Ronaldo mwaka 2018.
Kwa mujibu wa gazeti la Marca, Ronaldo baada ya kuona Modric ametwaa tuzo hiyo hakukubaliana naye huku akidai yeye ndiye aliyestahili kuchukua jambo ambalo Ramos alimjia juu Ronaldo.
Hivyo tangu hapo 2018, Ronaldo na Ramos walikuwa hawaongei, lakini juzi waliziweka tofauti zao pambeni na kuanza kuzungumza kama zamani.
Kwa kuthibitisha hilo, Ramos alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo huku wakiwa wamaishika jezi ya Ronaldo na pembeni yao akiwepo aliyewahi kuwa baki wa Madrid, Pep.
“Bado tupo pamoja… kuna mambo mengine yanakuja, nina furaha kukuona rafiki yangu,” aliandika Ramos kwenye picha hiyo.
Wawili hao wamekutana kwa mara ya kwanza tangu Ronalo alipoodoka Madrid mwaka 2018 na kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus. Ramos yeye ameendelea kubaki Real Madrid tangu alipojiunga mwaka 2005.
Safi