26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

BOCCO NJE STARS

 Na WINFRIDA MTOI, -DAR ES SALAAM 

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Etienne Ndayiragije, amemuondoa kikosini mshambuliaji John Bocco kutokana na hali yake kutoimarika. 

Bocco aliitwa katika kikosi hicho akiwa ametoka katika majeraha aliyopata wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba ilipocheza na Mtibwa Sugar, Septemba 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana, viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam, Ndayiragije, alisema maandalizi yanendelea vizuri na wachezaji wote wamewasili kambini, lakini Bocco ameonekana hayuko vizuri hivyo kumruhusu kuendelea na matibabu. 

Ngayiragije alisema kipindi alichofanya mazoezi, amepata kile alichohitaji kwa wachezaji hao, ikiwamo muunganiko na mchezo wa Jumapili, hivyo mtihani uliobaki kwao ni kufanya vizuri siku hiyo. 

“Mazoezi yanaendelea vizuri tangu tumeanza, lakini kuna tatizo kidogo limetokea kwa John Bocco, tumeona akaendelee tu na matibabu, pia nimeona picha niliyotarajia katika kikosi changu,” alisema. 

 Alisema kukosekana kwa mchezaji huyo ni pengo, lakini wapo wengine watapata nafasi akiamini wataitendea haki. 

Alisema Burundi ni kipimo kizuri kwao kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) kwa sababu soka wanalocheza linafanana na Tunisia watakayokutana nayo. 

“Aina ya uchezaji wa Burundi haitofautiani sana na Tunisia, naamini ni kipimo kizuri kwetu, Wanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kusapoti timu yao kama walivyofanya katika mechi zilizopita,” alisema. 

Katika hatua nyingine, winga wa Taifa Stars, Simon Msuva na beki Nickson Kibabage, wanaochezea Difaa El Jadid ya Morocco, wamewasili jana na kujiunga na wenzao. 

Akizungumza baada ya kuwasili, Msuva alisema amefurahi kujumuika na wenzake kwa sababu ni muda mrefu hawajaonana, hivyo amejipanga kupigania taifa lake. 

Msuva alisema kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa kila mara, inatengeneza historia ya maisha yake ya soka hapo baadaye. 

“Tumekaa muda mrefu kutokana na kipindi cha janga la corona, ila kiwango changu hakijashuka, tulirudi mazoezini na kuanza kucheza mechi za ligi ambao zote nimecheza, imebaki moja tumalize,” alisema Msuva. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles