22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

REDKNAPP: SINA UHAKIKA KWA CHELSEA KUTWAA TAJI LA ENGLAND

LONDON, ENGLAND


KOCHA wa zamani wa timu ya  Tottenham, Harry Redknapp, amesema kuwa hana uhakika wa vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, kama wanaweza kutwaa taji hilo licha ya kuongoza msimamo wa ligi hiyo.

Redknapp anaongeza kuwa katika mchezo uliochezwa juzi, anahisi kuwa kikosi cha kwanza cha Tottenham kilikuwa bora  zaidi ya wapinzani wao Chelsea licha ya kuambulia kichapo cha mabao 2-1.

Ushindi huo wa kikosi hicho cha Antonio Conte, uliwafanya warejee kileleni baada ya bao safi lililofungwa na Pedro Rodriguez pamoja na Victor Moses waliozima ndoto ya Tottenham waliokuwa wakiongoza kwa bao la dakika za mwanzoni lililofungwa na Christian Eriksen.

Hata hivyo, Redknapp anaeleza kuwa matokeo hayo yangekuwa tofauti kama kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino, angekuwa na  timu imara kwa muda wote na kuongeza kuwa iwapo kocha huyo atafanya maboresho katika kikosi hicho, wanaweza kutwaa taji hilo tangu mwaka 1961.

“ Inawezekana  Chelsea wakaendelea kuwa vinara wa ligi hiyo lakini bado inaendelea, hivyo ni vigumu kutabiri ubingwa kipindi hiki.

“Kama wachezaji wa Tottenham wakirejea, akiwamo Alderweireld na Rose, inaweza kuimarika zaidi katika mbio za ubingwa huo,” alisema Redknapp.

Kocha huyo alionesha wasiwasi wake kuhusu mfumo wa uchezaji wa Chelsea wa 3-4-3 kama utawasaidia kutwaa taji hilo msimu huu.

“Licha ya kikosi cha Conte kushinda michezo saba tangu wacheze mfumo huo na kufunga mabao 19, nina wasiwasi kama utawasaidia na kutwaa taji hilo msimu huu,” alisema Redknapp.

Redknapp alisema licha ya Chelsea kuongoza ligi hiyo na kuwa katika kiwango bora, wapo wachezaji wa kikosi cha kwanza hawafai kucheza kikosi chao cha kwanza.

“Nafikiri wachezaji watatu au wanne wa kikosi cha kwanza cha Chelsea hawana ubora wa kucheza katika kikosi hicho na kutoa msaada wa kushinda taji la ligi hiyo msimu huu.

“Miongoni mwa wachezaji hao ni beki wa kushoto, hata hivyo sifurahishwi na mabeki watatu wa kati, kwani sidhani kama wanafaa na kuwa na msaada katika eneo la kiungo wa timu hiyo wakati inapohitaji msaada,” alisema Redknapp.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles