24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

ARSENAL WAICHAPA BOURNAMOUTH 3-1

LONDON, ENGLAND


arsenalTIMU ya Arsenal jana ilifanikiwa kujikusanyia pointi tatu muhimu kwa kuinyuka timu ya Bournamouth mabao 3-1, katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Emirate.

Ushindi  huo  unaifanya Arsenal kuwa na ponti  28, ikiwa ni tofauti ya pointi tatu dhidi ya vinara wa ligi hiyo Chelsea wenye pointi 31.

Arsenal walionekana kuwa na presha ya ushindi wa mapema, baada ya wapinzani wao, Chelsea, Liverpool na Manchester City kushinda katika michezo yao ya Ligi Kuu England waliyocheza juzi.

Bournemouth walijaribu kucheza kwa ubora wao lakini walijikuta wakishindwa kuwazuia washambuliaji wa Arsenal kung’ara katika mchezo huo.

Arsenal ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 12 kupitia kwa mshambuliaji wake, Alexis Sánchez.

Hata hivyo, Callum Wilson alifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 23 kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Arsenal, Nacho Monreal, kumfanyia madhambi mchezaji huyo.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa timu hizo kuwa sare kwa bao 1-1.

Winga wa timu ya Arsenal, Theo Walcott, aliwanyanyua mashabiki wa timu hiyo dakika ya 53, baada ya kufunga bao la pili kwa kichwa kupitia pasi safi aliyopata kutoka kwa Monreal.

Dakika 90 Sanchez alifanikiwa kuongeza bao la tatu baada ya kupokea  pasi nzuri aliyopata kutoka kwa Mesut Ozil.

Bao hilo lilihitimisha kalamu ya mabao ambapo hadi kipyenga kinapulizwa dakika ya 90, Arsenal ilitoka kifua mbele kwa kushinda mabao 3-1.

Katika mchezo huo, Walcot alifunga bao lake la sita na kumzawadia mtoto wake wa pili aliyezaliwa Ijumaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles