26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

GUARDIOLA APANGA KUITIBULIA CHELSEA

LONDON, ENGLAND


01_26081858_7bf480_2710572aKOCHA wa timu ya Manchester City, Pep Guardiola, amekiri kutaka kutibua mipango ya mafanikio ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte, wakati watakapocheza na wapinzani wao hao katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Makocha hao wawili ni kati ya idadi ya makocha wenye majina makubwa katika Ligi ya England msimu huu na wameonekana kuhitaji matokeo makubwa hasa baada ya timu zao kufanya vibaya katika msimu uliopita.

Inadaiwa mashabiki wachache wanatarajia kuwa huenda Conte anaweza kung’ara mbele ya Guardiola katika hatua hii ambayo Mhispania huyo ndio anaonekana kuwa  kocha bora wa ligi hiyo.

Manchester City wanatarajia kuwakaribisha wapinzani wao Chelsea katika Uwanja wa Etihad, huku wakiwa na matarajio ya  kupata pointi tatu muhimu, huku Guardiola akithibitisha kuwa  kuna  kitu cha kujifunza kutoka kwa wapinzani wao hao.

“Sasa tunakwenda kucheza dhidi ya timu bora Ligi Kuu England,” alisema Guardiola baada ya kikosi chake kushinda dhidi ya Burnley hivi karibuni.

Kocha huyo aliongeza kuwa Chelsea katika michezo yao mitano au sita iliyopita walicheza vizuri, si tu walipata ushindi katika michezo hiyo, bali aina ya uchezaji wao ni wa kuvutia na wenye kuogopewa na wapinzani wao.

“Tunatakiwa kujaribu na kugundua siri ya Conte kufanya vizuri katika michezo yake ili kupata ushindi katika mchezo huo.

“Kwa sasa tuna siku sita au saba za  kujiandaa na mchezo huo, wachezaji wetu wengi wamechoka hivyo tunatakiwa kufanya tuwezalo ili kupata ushindi,” alieleza Guardiola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles