23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

TAMWA KUAZIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

edda
Edda Sanga

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzani – TAMWA kinaungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hasa watoto wa kike.

Kauli mbiu ya mwaka huu, ya “Funguka! Pinga Ukatili wa Kijinsia: Elimu Salama Kwa Wote”, inalenga kila mzazi, mlezi, ndugu, jamaa kwa kushirikiana na serikali kumlinda mtoto wa kike hasa anapokumbana na vizuizi vinavyodidimiza  ndoto yake ili aweze kufikia mafanikio.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga, amesisitiza kuwa kama sehemu ya maadhimisho hayo, TAMWA kupitia Kituo chake cha Usuluhishi (CRC) kinatoa huduma ya ushauri nasaha kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi na Newala Mkoani Mtwara.

“TAMWA itaendelea kutumia vyombo vya habari vikiwemo vya radio za jamii, runinga na magazeti kutoa elimu ya uelewa kwa jamii kuhusu vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto,” alisema Sanga

TAMWA inaamini kuwa ukatili wa kijinsia unaweza kupungua endapo wazazi, walezi, walimu, ndugu, jamaa wataona umuhimu wa kukemea vitendo hivyo kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha vyombo vya maamuzi vinalivalia njuga suala hili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles